Kumbukumbu la Sheria 3:21-22
Kumbukumbu la Sheria 3:21-22 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kisha nikamwamuru Yoshua, ‘Wewe umeona kwa macho yako mambo yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amewatendea wafalme hawa wawili, Sihoni na Ogu; basi, yeye atawatendea vivyo hivyo wafalme wa nchi zote mtakazopitia. Msiwaogope maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye atakayepigana kwa ajili yenu.’
Kumbukumbu la Sheria 3:21-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda BWANA, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda BWANA kila ufalme huko uvukiako. Msiwache, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye awapiganiaye.
Kumbukumbu la Sheria 3:21-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda BWANA, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda BWANA kila ufalme huko uvukiako. Msiwache, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye awapiganiaye.
Kumbukumbu la Sheria 3:21-22 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo BWANA Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. BWANA atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo. Msiwaogope, BWANA Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”