Kumbukumbu la Sheria 28:1-2
Kumbukumbu la Sheria 28:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
“Kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na kuzingatia kwa uangalifu amri ambazo ninawaamuru leo, yeye atawaweka juu ya mataifa yote duniani. Kama mkitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mtapewa baraka zifuatazo
Kumbukumbu la Sheria 28:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Sheria 28:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Sheria 28:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama ukimtii BWANA Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, BWANA Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia. Baraka hizi zote zitakuja juu yako na kukupata, kama ukimtii BWANA Mungu wako