Kumbukumbu la Sheria 27:9-16
Kumbukumbu la Sheria 27:9-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako. Basi isikize sauti ya BWANA, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo. Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema, Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini; na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali. Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu, Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Sheria 27:9-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, Mose pamoja na makuhani Walawi wakawaambia watu wote wa Israeli, “Nyamazeni mnisikilize enyi watu wa Israeli. Leo hii nyinyi mmekuwa watu wake Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kwa hiyo mtatii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu mkizifuata amri zake na masharti yake ambayo ninawaamuru leo.” Siku hiyo Mose aliwaagiza watu na kusema, “Mkisha vuka Yordani, makabila yafuatayo yatasimama juu ya mlima Gerizimu kuwabariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini. Na makabila yafuatayo yatasimama juu ya mlima Ebali wakati laana zitakapotolewa: Reubeni, Gadi, Asheri, Zebuluni, Dani na Naftali. Nao Walawi watawatangazia watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa: “ ‘Alaaniwe mtu yeyote afanyaye sanamu ya kuchonga au ya kusubu na kuisimamisha kwa siri, kitu ambacho kimetengenezwa na mikono ya fundi na ambacho ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayemdharau baba yake au mama yake.’ Na watu wote wataitika, ‘Amina!’
Kumbukumbu la Sheria 27:9-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako. Basi isikize sauti ya BWANA, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo. Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema, Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini; na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali. Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu, Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Sheria 27:9-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako. Basi isikize sauti ya BWANA, Mungu wako, ufanye maagizo yake na amri zake nikuagizavyo leo. Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema, Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini; na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali. Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu, Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Sheria 27:9-16 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kisha Musa na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Mtii Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.” Siku ile ile Musa akawaagiza watu: Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yusufu na Benyamini. Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali. Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa: “Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”