Kumbukumbu la Sheria 27:11-26
Kumbukumbu la Sheria 27:11-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku hiyo Mose aliwaagiza watu na kusema, “Mkisha vuka Yordani, makabila yafuatayo yatasimama juu ya mlima Gerizimu kuwabariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini. Na makabila yafuatayo yatasimama juu ya mlima Ebali wakati laana zitakapotolewa: Reubeni, Gadi, Asheri, Zebuluni, Dani na Naftali. Nao Walawi watawatangazia watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa: “ ‘Alaaniwe mtu yeyote afanyaye sanamu ya kuchonga au ya kusubu na kuisimamisha kwa siri, kitu ambacho kimetengenezwa na mikono ya fundi na ambacho ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayemdharau baba yake au mama yake.’ Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote aondoaye alama ya mpaka wa jirani yake.’ Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote ampotoshaye kipofu njiani.’ Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayepotosha haki ya mgeni au yatima au mjane’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mwanamume alalaye na mke wa baba yake, maana amemwaibisha baba yake’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote alalaye na mnyama yoyote’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote alalaye na dada yake awe ni binti ya baba yake au binti ya mama yake’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote alalaye na mama mkwe wake’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayeua mtu kwa siri’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote apokeaye hongo ili aue mtu asiye na hatia’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’ “ ‘Alaaniwe mtu yeyote asiyekubali maneno haya ya sheria na kuyatii’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’
Kumbukumbu la Sheria 27:11-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema, Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini; na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali. Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu, Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yoyote. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na dada yake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina. Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Sheria 27:11-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Musa akawaagiza wale watu siku iyo hiyo, akasema, Hawa na wasimame juu ya mlima wa Gerizimu kwa kuwabarikia watu, mkiisha vuka Yordani; Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Yusufu, na Benyamini; na hawa na wasimame juu ya mlima wa Ebali kwa laana; Reubeni, na Gadi, na Asheri, na Zabuloni, na Dani, na Naftali. Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu, Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina. Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina. Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Sheria 27:11-26 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Siku ile ile Mose akawaagiza watu: Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini. Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali. Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa: “Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.” Kisha watu wote watasema, “Amen!” “Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”