Kumbukumbu la Sheria 26:1-11
Kumbukumbu la Sheria 26:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
“Baada ya kufika na kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anawapa iwe yenu na kuishi huko, baadhi ya malimbuko ya mazao utakayovuna katika nchi anayokupa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, utayachukua katika kikapu mpaka pale mahali ambapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amepachagua pawe makao yake. Utamwendea kuhani anayehudumu wakati huo, na kumwambia, ‘Leo ninakiri mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, kuwa nimeingia katika nchi aliyowaapia wazee wetu kuwa atatupa.’ “Naye kuhani atakapochukua kikapu hicho mikononi mwako na kukiweka mbele ya madhabahu ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, utatamka maneno haya mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako: ‘Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyetangatanga huko na huko, kisha akashuka kwenda Misri akaishi huko kama mgeni. Yeye na jamaa yake walikuwa watu wachache tu walipokuwa huko, lakini wakawa taifa kubwa lenye nguvu na watu wengi. Wamisri walitutendea kwa ukatili wakatutesa na kutulazimisha kufanya kazi ngumu ya watumwa. Kisha tukamlilia Mwenyezi-Mungu, Mungu wa wazee wetu, akasikia kilio chetu, na kuyaona mateso yetu, kazi ngumu na dhuluma tulizozipata. Basi, Mwenyezi-Mungu akatutoa huko Misri kwa mkono wake wa nguvu ulionyoshwa, kwa vitisho, ishara na maajabu. Alituleta hapa na kutupatia nchi hii inayotiririka maziwa na asali. Na sasa ninamletea Mwenyezi-Mungu malimbuko ya mazao ya nchi ambayo amenipa.’ “Kisha utaweka kikapu chini, mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, na kuabudu mbele zake. Nawe utafurahia mema yote ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, amekujalia wewe na jamaa yako. Nao watafurahi pamoja nawe.
Kumbukumbu la Sheria 26:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na itakuwa, ukiisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi, na kuimiliki, na kukaa ndani yake; twaa malimbuko ya ardhi, utakayoyavuna katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako; ukayatie katika kikapu, ukaende hata mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wako, ili alikalishe jina lake huko. Ukamwendee kuhani atakayekuwapo siku zile, ukamwambie, Ninakiri leo kwa BWANA, Mungu wako, ya kuwa nimeingia katika nchi BWANA aliyowaapia baba zetu ya kwamba atatupa. Naye kuhani atakipokea kikapu mkononi mwako, akiweke chini mbele ya madhabahu ya BWANA, Mungu wako. Nawe ujibu, ukaseme mbele za BWANA, Mungu wako, Baba yangu alikuwa Mwarami karibu na kupotea, akashuka Misri, akakaa huko ugenini, nao ni wachache hesabu yao; akawa taifa kubwa huko, yenye nguvu na watu wengi. Wamisri wakatuonea, wakatutesa, wakatutumikisha utumwa mzito. Tukamlilia BWANA, Mungu wa baba zetu; BWANA akasikia sauti yetu, akaona na taabu yetu, na kazi yetu, na kuonewa kwetu. BWANA akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mwingi, na kwa ishara, na kwa maajabu; naye ametuingiza mahali hapa, na kutupa nchi hii, nchi ijaayo maziwa na asali. Na sasa, tazama, nimeleta malimbuko ya mazao ya ardhi uliyonipa, Ee BWANA. Kisha ukiweke chini mbele za BWANA, Mungu wako, ukasujudu mbele za BWANA, Mungu wako; ukayafurahie mema yote ambayo BWANA, Mungu wako, amekupa, na nyumba yako, wewe, na Mlawi, na mgeni aliye kati yako.
Kumbukumbu la Sheria 26:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Kumbukumbu la Sheria 26:1-11 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mtakapokuwa mmeingia nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa kama urithi na mtakapokuwa mmeimiliki na kukaa ndani yake, chukueni baadhi ya mavuno ya kwanza ya yale yote mtakayozalisha kutoka udongo wa nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa na mweke kwenye kapu. Kisha uende mahali Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakapopachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina lake, na umwambie kuhani atakayekuwepo wakati huo, “Ninatangaza leo kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwamba nimekuja katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.” Kuhani atapokea lile kapu mikononi mwako na kuliweka chini mbele ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Kisha utatangaza mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu. Kisha tulimlilia Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zetu, naye Mwenyezi Mungu akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu. Akatuleta mahali hapa akatupatia nchi hii, nchi inayotiririka maziwa na asali; nami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umenipa.” Weka kapu mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na usujudu mbele zake. Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walio miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu.