Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Sheria 19:15-21 - Compare All Versions

Kumbukumbu la Sheria 19:15-21 BHN (Biblia Habari Njema)

“Ushahidi wa mtu mmoja hautoshi kumhukumu mtu juu ya kosa lolote la jinai au uovu kuhusu kosa lolote alilofanya. Ni ushahidi wa watu wawili au watatu tu ndio utakaothaminiwa. Ikiwa shahidi mdhalimu atatokea kumshtaki mtu yeyote juu ya kosa fulani, basi yeye na mshtakiwa kuhusu mzozo huo watakwenda mbele ya Mwenyezi-Mungu, mbele ya makuhani na waamuzi ambao wako katika ofisi wakati huo; waamuzi watachungua kwa uangalifu kesi hiyo na ikiwa mshahidi ni mshahidi wa uongo na amemshtaki mwenzake kwa uongo, basi, mtamtendea alivyokusudia kumtendea ndugu yake. Ndivyo mtakavyokomesha uovu kati yenu. Nao watu wengineo watasikia na kuogopa, na uovu kama huo hautafanyika tena kati yenu. Msiwaonee huruma watu wa aina hiyo. Uhai utalipwa kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono na mguu kwa mguu.

Kumbukumbu la Sheria 19:15-21 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wowote, wala kwa dhambi yoyote, katika makosa akosayo yoyote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu. Shahidi mdhalimu akimwinukia mtu yeyote na kushuhudia juu yake ya upotoe; ndipo wale watu washindanao kwa mambo yale na wasimame wote wawili mbele za BWANA, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo; nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye; ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Kumbukumbu la Sheria 19:15-21 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wo wote, wala kwa dhambi yo yote, katika makosa akosayo yo yote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu. Shahidi mdhalimu akimwinukia mtu ye yote na kushuhudia juu yake ya upotoe; ndipo wale watu washindanao kwa mambo yale na wasimame wote wawili mbele za BWANA, mbele ya makuhani na waamuzi watakaokuwapo siku hizo; nao waamuzi na watafute kwa bidii; na tazama, yule shahidi akiwa shahidi wa uongo, naye ametoa ushahidi wa uongo juu ya nduguye; ndipo mtamfanyia kama alivyodhani kumfanyia nduguye; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako. Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Kumbukumbu la Sheria 19:15-21 NEN (Neno)

Shahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lolote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lolote lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu. Kama shahidi mwenye nia ya kumdhuru mwingine akisimama kumshtaki mtu kwa uhalifu, watu wawili wanaohusika katika mabishano lazima wasimame mbele za BWANA na mbele ya makuhani na waamuzi ambao wako kazini wakati huo. Waamuzi lazima wafanye uchunguzi kwa makini na shahidi akionekana kuwa ni mwongo, akitoa ushuhuda wa uongo dhidi ya ndugu yake, basi mtende kama alivyotaka kumtendea ndugu yake. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu. Watu watakaosalia watasikia hili na kuogopa, uovu kama huo kamwe hautatendeka tena miongoni mwenu. Msioneshe huruma, uhai kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.