Kumbukumbu la Sheria 18:14-22
Kumbukumbu la Sheria 18:14-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, BWANA, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo. BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Kama vile ulivyotaka kwa BWANA, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya BWANA, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa. BWANA akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena BWANA? Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope
Kumbukumbu la Sheria 18:14-22 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mataifa haya ambayo mtaimiliki nchi yao hufuata maongozi ya waaguzi na wapiga ramli; lakini Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu hawaruhusu nyinyi kufanya hivyo. “Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawateulieni nabii aliye kama mimi kutoka miongoni mwenu, nanyi mtamsikiliza huyo. Hicho ndicho mlichomwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kule Horebu, siku ile mlipokusanyika na kusema, ‘Tusisikie tena sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala tusiuone tena moto huu mkubwa, tusije tukafa!’ Naye Mwenyezi-Mungu akaniambia, ‘Wamesema ukweli. Nitawateulia miongoni mwa ndugu zao wenyewe nabii kama wewe; nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Yeyote ambaye hatasikia maneno atakayosema nabii huyo kwa jina langu, mimi mwenyewe nitamwadhibu. Lakini nabii yeyote atakayesema kwa jina la miungu mingine, au atakayejaribu kusema neno kwa jina langu hali mimi sikumwambia aseme, huyo nabii atakufa.’ “Lakini nyinyi mwaweza kusema, ‘Tutawezaje kutambua neno ambalo Mwenyezi-Mungu hakulisema?’ Kama nabii akisema kitu ati kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kitu hicho hakifanyiki au hakiwi kweli, jambo hilo hakulisema Mwenyezi-Mungu; nabii amelisema kwa ufidhuli, nanyi msitishwe na jambo hilo.
Kumbukumbu la Sheria 18:14-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, BWANA, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo. BWANA, Mungu wako, atakupa nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Kama vile ulivyotaka kwa BWANA, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya BWANA, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa. BWANA akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. Mimi niwaiwanulia nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena BWANA? Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope.
Kumbukumbu la Sheria 18:14-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, BWANA, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo. BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Kama vile ulivyotaka kwa BWANA, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya BWANA, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa. BWANA akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema. Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake. Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa. Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena BWANA? Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope
Kumbukumbu la Sheria 18:14-22 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini ninyi, Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, hajawaruhusu kufanya hivyo. Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye. Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.” Mwenyezi Mungu akaniambia: “Wanachosema ni vyema. Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru. Kama mtu yeyote hatasikiliza maneno yangu ambayo huyo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha. Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu chochote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.” Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa na Mwenyezi Mungu?” Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la Mwenyezi Mungu hakikutendeka au kutimia, huo ni ujumbe ambao Mwenyezi Mungu hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.