Kumbukumbu la Sheria 16:18-20
Kumbukumbu la Sheria 16:18-20 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mtateua waamuzi na maofisa kutoka makabila yenu katika miji yenu ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa, nao watatoa hukumu za haki kwa watu. Msipotoshe haki; msiwe na upendeleo, wala msikubali kupokea rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya watu wenye hekima na kupotosha kesi ya mtu mwadilifu. Mtazingatia haki tu, ili mpate kuishi na kuimiliki nchi mnayopewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Kumbukumbu la Sheria 16:18-20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambao BWANA Mungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa. Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki. Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo BWANA Mungu wenu anawapa.
Kumbukumbu la Sheria 16:18-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Weka waamuzi na maofisa katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki. Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki. Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Kumbukumbu la Sheria 16:18-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Weka waamuzi na maakida katika malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako, kwa hesabu ya kabila zako; nao wawaamue watu kwa maamuzi ya haki. Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki. Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.