Kumbukumbu la Sheria 16:16
Kumbukumbu la Sheria 16:16 Biblia Habari Njema (BHN)
“Wanaume wote wa taifa lenu watakuja mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mara tatu kila mwaka, mahali atakapopachagua: Wakati wa sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, sikukuu ya kuvuna majuma na wakati wa sikukuu ya vibanda. Wasiende mbele ya Mwenyezi-Mungu mikono mitupu.
Kumbukumbu la Sheria 16:16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mara tatu kwa mwaka na watokee wana wa kiume wako wote mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu.
Kumbukumbu la Sheria 16:16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mara tatu kwa mwaka na watokee wanawaume wako wote mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu.
Kumbukumbu la Sheria 16:16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele za BWANA Mungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele za BWANA mikono mitupu