Kumbukumbu la Sheria 11:20-21
Kumbukumbu la Sheria 11:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Ziandikeni katika vizingiti vya nyumba zenu, na katika malango yenu, ili nyinyi na watoto wenu mpate kuishi maisha marefu katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliapa kuwapa babu zenu, siku zote mbingu zitakapodumu juu ya dunia.
Kumbukumbu la Sheria 11:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.
Kumbukumbu la Sheria 11:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.
Kumbukumbu la Sheria 11:20-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu, ili kwamba siku zenu na siku za watoto wenu zipate kuwa nyingi katika nchi ile BWANA aliyoapa kuwapa baba zenu, kama zilivyo nyingi siku za mbingu juu ya nchi.