Danieli 8:19-21
Danieli 8:19-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha akaniambia, ‘Sikiliza, ninakufahamisha matokeo ya ghadhabu ya Mungu yatakavyokuwa. Maono hayo yanahusu wakati wa mwisho. “ ‘Yule kondoo dume uliyemwona mwenye pembe mbili, ni wafalme wa Media na Persia. Yule beberu ni mfalme wa Ugiriki. Ile pembe kubwa katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
Danieli 8:19-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa. Yule kondoo dume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi. Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Ugiriki; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
Danieli 8:19-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa. Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi. Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
Danieli 8:19-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Akaniambia, “Nitakuambia yale yatakayotokea baadaye wakati wa ghadhabu, kwa sababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho ulioamriwa. Kondoo dume mwenye pembe mbili ambaye ulimwona anawakilisha wafalme wa Umedi na Uajemi. Yule beberu mwenye nywele nyingi ni mfalme wa Uyunani, nayo ile pembe ndefu katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.