2 Samueli 6:1-10
2 Samueli 6:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Daudi akakusanya tena wateule wote wa Israeli, watu thelathini elfu. Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la BWANA wa majeshi akaaye juu ya makerubi. Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyoko kilimani, pamoja na sanduku la BWANA; na huyo Ahio akatangulia mbele ya sanduku. Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi. Hata walipofika kwa uga ya Nakoni, Uza akalinyoshea mkono sanduku la Mungu, akalikamata kwa maana wale ng’ombe walikunguwaa. Ndipo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Uza; naye Mungu akampiga huko kwa kosa lake; hata akafa pale pale penye sanduku la Mungu. Daudi akaona uchungu kwa kuwa BWANA amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo. Naye Daudi akamwogopa BWANA siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la BWANA? Basi Daudi hakutaka kulileta sanduku la BWANA kwake mjini mwa Daudi; ila Daudi akalihamisha nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti.
2 Samueli 6:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa mara nyingine, Daudi aliwakusanya wale askari bora wa Israeli, jumla yao 30,000. Daudi aliondoka akaenda pamoja na watu wake wote aliokuwa nao kutoka Baala-yuda, kwenda kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa. Basi, wakalichukua sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Abinadabu iliyokuwa mlimani, wakalibeba juu ya gari jipya. Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakawa wanaliendesha gari hilo jipya, likiwa na sanduku hilo la Mungu, naye Ahio akiwa anatangulia mbele ya sanduku hilo. Daudi na watu wote wa Israeli, wakawa wanaimba nyimbo na kucheza kwa nguvu zao zote, mbele ya Mwenyezi-Mungu. Walipiga ala za muziki zilizotengenezwa kwa mvinje: Vinubi, vinanda, matari, kayamba na matoazi. Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Nakoni, Uza aliunyosha mkono wake na kulishika sanduku la Mungu kwa sababu wale ng'ombe walijikwaa. Hapo, hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi ya Uza. Mungu akamuua palepale. Uza akafa papo hapo kando ya sanduku la Mungu. Naye Daudi alikasirika kwa kuwa Mwenyezi-Mungu alimwadhibu Uza kwa hasira. Hivyo, mahali hapo pakaitwa Peres-uza mpaka hivi leo. Siku hiyo Daudi alimwogopa Mwenyezi-Mungu akasema, “Sasa litanijiaje sanduku la Mwenyezi-Mungu?” Kwa hiyo, Daudi hakuwa tayari kulipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu ndani ya mji wa Daudi, bali Daudi alilipeleka nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti.
2 Samueli 6:1-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Daudi akakusanya tena wateule wote wa Israeli, watu elfu thelathini. Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la BWANA wa majeshi akaaye juu ya makerubi. Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyoko kilimani, pamoja na sanduku la BWANA; na huyo Ahio akatangulia mbele ya sanduku. Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi. Hata walipofika kwenye uga wa Nakoni, Uza akalinyoshea mkono sanduku la Mungu, akalikamata kwa maana wale ng'ombe walijikwaa. Ndipo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Uza; naye Mungu akampiga huko kwa kosa lake; hata akafa pale pale penye sanduku la Mungu. Daudi akaona uchungu kwa kuwa BWANA amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo. Naye Daudi akamwogopa BWANA siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la BWANA? Basi Daudi hakutaka kulileta sanduku la BWANA kwake mjini mwa Daudi; ila Daudi akalihamisha nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti.
2 Samueli 6:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Daudi akakusanya tena wateule wote wa Israeli, watu thelathini elfu. Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la BWANA wa majeshi akaaye juu ya makerubi. Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyoko kilimani, pamoja na sanduku la BWANA; na huyo Ahio akatangulia mbele ya sanduku. Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi. Hata walipofika kwa uga ya Nakoni, Uza akalinyoshea mkono sanduku la Mungu, akalikamata kwa maana wale ng’ombe walikunguwaa. Ndipo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Uza; naye Mungu akampiga huko kwa kosa lake; hata akafa pale pale penye sanduku la Mungu. Daudi akaona uchungu kwa kuwa BWANA amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo. Naye Daudi akamwogopa BWANA siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la BWANA? Basi Daudi hakutaka kulileta sanduku la BWANA kwake mjini mwa Daudi; ila Daudi akalihamisha nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti.
2 Samueli 6:1-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Tena Daudi akakusanya watu 30,000 wa Israeli waliochaguliwa. Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la BWANA Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku. Wakaweka hilo Sanduku la Mungu juu ya gari jipya la kukokotwa na kulileta kutoka nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wana wa Abinadabu, walikuwa wakiongoza hilo gari jipya la kukokotwa likiwa na Sanduku la Mungu juu yake, naye Ahio alikuwa anatembea akiwa mbele yake. Daudi na nyumba yote ya Israeli walikuwa wanacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, vinubi, zeze, matari, kayamba na matoazi. Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Nakoni, Uza akanyoosha mkono na kulishika Sanduku la Mungu kwa sababu maksai walijikwaa. Hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Uza kwa sababu ya kitendo chake cha kukosa heshima, kwa hiyo Mungu akampiga akafia papo hapo kando ya Sanduku la Mungu. Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu ya BWANA ilifurika dhidi ya Uza, hivyo hadi leo mahali hapo panaitwa Peres-Uza. Daudi akamwogopa BWANA siku ile, akasema, “Ni jinsi gani Sanduku la BWANA litakavyoweza kunijia?” Hakuwa radhi kulichukua Sanduku la BWANA kwake katika Mji wa Daudi. Badala yake akalipeleka kwenye nyumba ya Obed-Edomu, Mgiti.