2 Wakorintho 12:8-9
2 Wakorintho 12:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Nilimsihi Bwana mara tatu kuhusu jambo hili ili linitoke. Lakini akaniambia: “Neema yangu inatosha kwa ajili yako; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu.” Basi, ni radhi kabisa kujivunia udhaifu wangu ili uwezo wake Kristo ukae juu yangu.
2 Wakorintho 12:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa ajili ya kitu hicho nilimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
2 Wakorintho 12:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
2 Wakorintho 12:8-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa habari ya jambo hili nilimsihi Bwana mara tatu aniondolee mwiba huu. Lakini aliniambia, “Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu.” Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.