2 Mambo ya Nyakati 32:32-33
2 Mambo ya Nyakati 32:32-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na matendo yake mema, tazama, yameandikwa katika maono ya nabii Isaya, mwana wa Amozi, katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli. Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.
2 Mambo ya Nyakati 32:32-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Matendo mengine ya mfalme Hezekia na wema wake, yameandikwa katika Maono ya nabii Isaya mwana wa Amozi, katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli. Hezekia alifariki dunia na kuzikwa kwenye sehemu ya juu ya makaburi ya wafalme. Watu wote wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu walimtolea heshima kuu wakati wa kifo chake, naye Manase, mwanawe, akatawala mahali pake.
2 Mambo ya Nyakati 32:32-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na matendo yake mema, tazama, yameandikwa katika maono ya Isaya nabii, mwana wa Amozi, katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.
2 Mambo ya Nyakati 32:32-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Matukio mengine ya utawala wa Hezekia na matendo yake ya kujitoa kwa moyo yameandikwa katika maono ya nabii Isaya mwana wa Amozi kwenye kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Hezekia akalala na baba zake na akazikwa kwenye kilima mahali yalipo makaburi ya wazao wa Daudi. Yuda wote na watu wa Yerusalemu wakamheshimu alipofariki. Naye Manase mwanawe akawa mfalme baada yake.