2 Mambo ya Nyakati 26:16
2 Mambo ya Nyakati 26:16 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati mfalme Uzia alipokuwa na nguvu, alijaa kiburi ambacho kilisababisha maangamizi yake. Alimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wake kwa kuingia hekaluni akikusudia kufukiza ubani madhabahuni.
2 Mambo ya Nyakati 26:16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi BWANA, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
2 Mambo ya Nyakati 26:16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukuka, hata akafanya maovu, akamwasi BWANA, Mungu wake; kwani aliingia hekaluni mwa BWANA, ili afukize uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.
2 Mambo ya Nyakati 26:16 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa Mwenyezi Mungu ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba.