1 Wathesalonike 5:9-11
1 Wathesalonike 5:9-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa. Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, kama mnavyofanya sasa.
1 Wathesalonike 5:9-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye. Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

1 Wathesalonike 5:9-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa Mungu hakutuweka ili tupate hasira yake, bali ili tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tunakesha au tunalala. Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, hakika kama mnavyofanya.
1 Wathesalonike 5:9-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala. Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.