1 Wathesalonike 5:2-4
1 Wathesalonike 5:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo. Lakini nyinyi, ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi.
1 Wathesalonike 5:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana ninyi wenyewe mnajua hakika ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. Bali ninyi, ndugu, hamko gizani, hata siku ile iwapate kama mwizi.
1 Wathesalonike 5:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
1 Wathesalonike 5:2-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajapo usiku. Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka. Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi.