1 Samueli 7:3
1 Samueli 7:3 Biblia Habari Njema (BHN)
Samueli akawaambia Waisraeli, “Kama mnamrudia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wenu wote, ni lazima mwondoe kati yenu miungu ya kigeni na sanamu za Ashtarothi. Mwelekeeni Mwenyezi-Mungu kwa moyo wote, na kumtumikia yeye peke yake; naye atawaokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti.”
1 Samueli 7:3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamwelekezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.
1 Samueli 7:3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.
1 Samueli 7:3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Naye Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, “Ikiwa mtamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi iacheni miungu migeni na Maashtorethi na kujitoa wenyewe kwa BWANA na kumtumikia yeye peke yake, naye atawaokoa ninyi na mkono wa Wafilisti.”