1 Samueli 20:11-16
1 Samueli 20:11-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Yonathani akamjibu, “Njoo twende shambani!” Basi, wakaenda. Yonathani akamwambia Daudi, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, na awe shahidi yetu. Kesho au kesho kutwa, wakati kama huu nitamwuliza baba yangu. Ikiwa msimamo wake juu yako ni mzuri nitakueleza. Mwenyezi-Mungu na aniue ikiwa Shauli anakusudia kukudhuru, nami nisikutahadharishe ili uende mahali mbali ambapo utakuwa salama. Mwenyezi-Mungu na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. Ikiwa nitaendelea kuwa hai basi, nioneshe ule upendo thabiti wa Mwenyezi-Mungu, ili nisife, tena usiache kuitendea jamaa yangu kwa uaminifu milele. Na Mwenyezi-Mungu atakapowakatilia mbali adui zako kutoka duniani, naomba na jina langu lisikatiliwe mbali kutoka jamaa yako. Mwenyezi-Mungu awalipize kisasi adui zako.”
1 Samueli 20:11-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yonathani akamwambia Daudi, Twende zetu nje mashambani. Wakatoka wote wawili, wakaenda mashambani. Naye Yonathani akamwambia Daudi, BWANA, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili? BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukutuma uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. Nawe utanionesha fadhili za BWANA, ili nisife, si wakati huu tu maadamu mimi ni hai; lakini pamoja na hayo, hata jamaa yangu pia hutawaondolea kabisa fadhili zako; la, hata wakati ule BWANA atakapokuwa amewaondoa kabisa adui za Daudi wote pia katika uso wa nchi. Basi Yonathani akafanya agano na jamaa yake Daudi, akisema, BWANA na awalipize kisasi adui zake Daudi.
1 Samueli 20:11-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yonathani akamwambia Daudi, Twende zetu nje mashambani. Wakatoka wote wawili, wakaenda mashambani. Naye Yonathani akamwambia Daudi, BWANA, Mungu wa Israeli, na awe shahidi; nitakapokuwa nimekwisha kumwuliza baba yangu, kama wakati huu kesho, au siku ya tatu, angalia, kama liko neno jema la kumfaa Daudi, je! Nisikupelekee habari na kukufunulia neno hili? BWANA anitende mimi, Yonathani, hivyo, na kuzidi, ikiwa yampendeza babangu kukutenda mabaya, nisipokufunulia haya, na kukupeleka uende zako kwa amani; na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. Nawe utanionyesha fadhili za BWANA, ili nisife, si wakati huu tu maadamu mimi ni hai; lakini pamoja na hayo, hata jamaa yangu pia hutawaondolea kabisa fadhili zako; la, hata wakati ule BWANA atakapokuwa amewaondoa kabisa adui za Daudi wote pia katika uso wa nchi. Basi Yonathani akafanya agano na jamaa yake Daudi, akisema, BWANA naye atayataka mkononi mwa adui zake Daudi.
1 Samueli 20:11-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja. Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha? Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, BWANA na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. BWANA na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. Lakini nitendee wema usiokoma kama ule wa BWANA siku zote za maisha yangu, ili nisije nikauawa, wala usiuondoe wema wako kwa jamaa yangu, hata kama ni wakati ule BWANA atakapokuwa amekatilia mbali kila adui wa Daudi kutoka kwenye uso wa dunia.” Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi, akisema: “BWANA na awaangamize adui za Daudi.”