1 Wafalme 8:44-45
1 Wafalme 8:44-45 Biblia Habari Njema (BHN)
“Watu wako wakienda vitani kupigana na adui yao kokote kule utakakowapeleka, nao wakikuomba wakielekea mji uliouchagua na nyumba niliyoijenga kwa ajili ya jina lako, nakusihi usikie sala yao na maombi yao huko mbinguni, uwapatie ushindi vitani.
1 Wafalme 8:44-45 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yoyote utakayowapeleka, wakikuomba, BWANA, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; basi, uyasikie huko mbinguni maombi yao na dua yao, ukaitetee haki yao.
1 Wafalme 8:44-45 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yo yote utakayowapeleka, wakikuomba, BWANA, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; basi, uyasikie huko mbinguni maombi yao na dua yao, ukaitetee haki yao.
1 Wafalme 8:44-45 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Wakati watu wako watakapokwenda vitani dhidi ya adui zao, popote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwa BWANA kuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, basi usikie dua na maombi yao kutoka mbinguni, ukawatetee haki yao.