1 Wafalme 7:13-14
1 Wafalme 7:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mfalme Sulemani akatuma watu kumleta Huramu kutoka Tiro. Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila ya Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, mstadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikilia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
1 Wafalme 7:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha mfalme Solomoni alimwita Hiramu kutoka Tiro. Huyo, alikuwa mwana wa mjane wa kabila la Naftali, na baba yake alikuwa mkazi wa Tiro, mfua shaba. Hiramu alikuwa na hekima nyingi na akili, na fundi stadi wa kazi yoyote ya shaba. Basi, alikuja kwa mfalme Solomoni, akamfanyia kazi yake yote.
1 Wafalme 7:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mfalme Sulemani akatuma watu kumleta Hiramu kutoka Tiro. Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
1 Wafalme 7:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mfalme Solomoni akatuma watu Tiro kumleta Hiramu, ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Solomoni na kufanya kazi zake zote alizopangiwa.