1 Wafalme 21:25-26
1 Wafalme 21:25-26 Biblia Habari Njema (BHN)
(Hakuna mtu aliyenuia kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kama Ahabu, ambaye alishawishiwa na Yezebeli, mkewe. Alitenda machukizo kwa kuabudu sanamu za miungu kama walivyofanya Waamori ambao hapo awali Mwenyezi-Mungu aliwafukuza mbele ya watu wa Israeli).
1 Wafalme 21:25-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
(Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa BWANA ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)
1 Wafalme 21:25-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
(Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa BWANA ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.)
1 Wafalme 21:25-26 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
(Hapajapata kamwe kuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza mwenyewe kutenda uovu machoni mwa BWANA, akiwa anachochewa na Yezebeli mkewe. Alitenda kwa uovu sana katika kuabudu sanamu, kama wale Waamori ambao BWANA aliowafukuza mbele ya Israeli.)