1 Wafalme 18:1-2
1 Wafalme 18:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Ikawa baada ya siku nyingi, mnamo mwaka wa tatu wa ukame, neno hili la Mwenyezi-Mungu likamjia Elia: “Nenda ukajioneshe kwa mfalme Ahabu, halafu nitanyesha mvua nchini.” Basi, Elia akaenda kujionesha kwa Ahabu. Wakati huo, njaa ilikuwa kali sana huko Samaria.
1 Wafalme 18:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa baada ya siku nyingi, neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu, kusema, Nenda, ukajioneshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi. Basi Eliya akaenda ili ajioneshe kwa Ahabu. Na njaa ilikuwa nzito katika Samaria.
1 Wafalme 18:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa baada ya siku nyingi, neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu, kusema, Enenda, ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi. Basi Eliya akaenda ili ajionyeshe kwa Ahabu. Na njaa ilikuwa nzito katika Samaria.
1 Wafalme 18:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Baada ya muda mrefu, katika mwaka wa tatu, neno la BWANA likamjia Eliya kusema, “Nenda ukajionyeshe kwa Ahabu na mimi nitanyesha mvua juu ya nchi.” Kwa hiyo Eliya akaenda kujionyesha kwa Ahabu. Wakati huu njaa ilikuwa kali sana katika Samaria