1 Yohane 1:7,9
1 Yohane 1:7 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini tukiishi katika mwanga, kama naye alivyo katika mwanga, basi, tutakuwa na umoja sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwanae, inatutakasa dhambi zote.
1 Yohane 1:9 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote.
1 Yohane 1:7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
1 Yoh 1:9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
1 Yohane 1:7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
bali tukienenda katika nuru, kama yeye alivyo katika nuru, tunashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
1 Yohana 1:9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.
1 Yohane 1:7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.