1 Wakorintho 12:24-25
1 Wakorintho 12:24-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; ili kusiwe na mgawanyiko katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe.
1 Wakorintho 12:24-25 Biblia Habari Njema (BHN)
ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwa heshima, ili kusiweko na utengano katika mwili, bali viungo vyote vishughulikiane.
1 Wakorintho 12:24-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe.
1 Wakorintho 12:24-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
wakati vile viungo vyenye uzuri havihitaji utunzaji wa pekee. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile vilivyopungukiwa, ili pasiwe na mafarakano katika mwili, bali viungo vyote vihudumiane kwa usawa kila kimoja na mwenzake.