1 Wakorintho 1:2
1 Wakorintho 1:2 Biblia Habari Njema (BHN)
tunawaandikia nyinyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho. Nyinyi mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana wao na wetu pia.
1 Wakorintho 1:2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
1 Wakorintho 1:2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
1 Wakorintho 1:2 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kwa kundi la waumini wa Mungu walioko Korintho, kwa wale waliotakaswa katika Al-Masihi Isa na walioitwa kuwa watakatifu, pamoja na wale wote ambao kila mahali wanaliitia Jina la Al-Masihi Isa Bwana wetu, aliye Bwana wao na wetu pia.