Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 8:1-40

1 Mambo ya Nyakati 8:1-40 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza, Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu, Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano. Wana wa Bela walikuwa: Adari, Gera, Abihudi, Abishua, Naamani, Ahoa, Gera, Shefufani na Huramu. Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi: Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni. Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara. Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao. Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali. Wana wa Elpaali walikuwa: Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka), na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi. Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi, Zebadia, Aradi, Ederi, Mikaeli, Ishpa, na Yoha. Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali. Yakimu, Zikri, Zabdi, Elienai, Silethai, Elieli, Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei. Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli, Abdoni, Zikri, Hanani, Hanania, Elamu, Anthothiya, Ifdeya na Penueli. Shamsherai, Sheharia, Athalia, Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu. Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu. Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka. Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, Gedori, Ahio, Zekeri, na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu. Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali. Yonathani akamzaa: Merib-Baali, naye Merib-Baali akamzaa Mika. Wana wa Mika walikuwa: Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi. Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli. Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao: Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli. Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa: Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150. Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.

1 Mambo ya Nyakati 8:1-40 Biblia Habari Njema (BHN)

Benyamini alikuwa na wana watano: Bela, mzaliwa wake wa kwanza, Ashbeli wa pili, Ahara wa tatu, Noha wa nne na Rafa wa tano. Bela naye alikuwa na wana: Adari, Gera, Abihudi, Abishua, Naamani, Ahoa, Gera, Shufamu na Huramu. Hawa ndio wazawa wa Ehudi. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa za wale waliokuwa wakiishi Geba, lakini wakachukuliwa mateka uhamishoni Manahathi; Naamani, Ahiya na Gera. Gera, baba yake Uza na Ahihudi, ndiye aliyewaongoza kuchukua hatua hiyo. Shaharaimu aliwapa talaka wake zake wawili, Hushimu na Baara na baadaye alipata watoto wa kiume nchini Moabu. Alimwoa Hodeshi, naye akamzalia wana saba: Yoabu, Sibia, Mesha, Malkamu, Yeuzi, Sakia, na Mirma. Hawa wanawe wote walikuja kuwa wakuu wa koo. Shaharaimu na mkewe Hushimu alipata wana wengine wawili: Abitubu na Elpaali. Wana wa Elpaali walikuwa watatu: Eberi, Mishamu na Shemedi ambaye aliijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji kandokando yake. Beria na Shema walikuwa miongoni mwa jamaa ambazo zilikuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na kuwafukuza wenyeji wa Gathi. Nao Ahio, Shashaki, Yeremothi, Zebadia, Aradi, Ederi, Mikaeli, Ishpa na Yoha ni wazawa wengine wa Beria. Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, Ishnerai, Izlia na Yobabu walikuwa wazawa wa Epaali. Yakimu, Zikri, Zabdi, Elienai, Zilethai, Elieli, Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wazawa wa Shimei. Ishpani, Eberi, Elieli, Abdoni, Zikri, Hanani, Hanania, Elamu, Anthothiya, Ifdeya na Penueli walikuwa wazawa wa Shashaki. Shamsherai, Sheharia, Athalia, Yaareshia, Elia na Zikri walikuwa baadhi ya wazawa wa Yerohamu. Hao ndio waliokuwa wakuu wa koo zao kulingana na vizazi vyao. Walikuwa wakuu na waliishi Yerusalemu. Yeieli, alikuwa mwanzilishi wa mji wa Gibeoni. Mkewe alikuwa Maaka. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Abdoni. Wanawe wengine ni Zuri, Kishi, Baali, Nadabu, Gedori, Ahio, Zekeri, na Miklothi baba yake Shimea. Hawa pia waliishi Yerusalemu karibu na watu wengine wa ukoo wao. Neri alimzaa Kishi, Kishi akamzaa Shauli. Shauli alikuwa na wana wanne: Yonathani, Malki-shua, Abinadabu na Eshbaali. Yonathani alimzaa Merib-baali, na Merib-baali akamzaa Mika. Mika alikuwa na wana wanne: Pithoni, Meleki, Terea na Ahazi. Ahazi alimzaa Yehoada. Naye Yehoada aliwazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri. Zimri alimzaa Mosa. Mosa alimzaa Binea, aliyemzaa Rafa, aliyemzaa Eleasa, naye Eleasa akamzaa Aseli. Wana wa Aseli walikuwa sita: Majina yao ni Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Aseli. Nao wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa watatu. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. Wana wa Ulamu walikuwa watu mashujaa sana wa vita, na wapiga upinde hodari. Alikuwa na wana na wajukuu wengi, jumla150. Hao wote waliotajwa hapo juu walikuwa wa ukoo wa Benyamini.

1 Mambo ya Nyakati 8:1-40 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Naye Benyamini akamzaa Bela, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Ashbeli, na wa tatu Ahiramu; na wa nne Noha, na wa tano Rafa. Na Bela alikuwa na wana; Adari, na Gera, na Abihudi; na Abishua, na Naamani, na Ahoa; na Gera, na Shufamu, na Huramu. Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi; na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi. Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara. Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu; na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao. Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali. Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake; na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi. Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi; na Zebadia, na Aradi, na Ederi; na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria. Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi; na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali. Na Yakimu, na Zikri, na Zabdi; na Elienai, na Silethai, na Elieli; na Adaya, na Beraya, na Shimrathi; walikuwa wana wa Shema. Na Ishpani, na Eberi, na Elieli; na Abdoni, na Zikri, na Hanani; na Hanania, na Elamu, na Anthothiya; na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki. Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia; na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu. Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu. Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka; na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni, na Suri, na Kishi, na Baali, na Nadabu; na Gedori, na Ahio, na Zekaria, Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao. Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali. Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika. Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi. Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa; na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli; naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli. Na wana wa Esheki nduguye ni hawa; mzaliwa wake wa kwanza, Ulamu, na wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti. Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia moja na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini.

1 Mambo ya Nyakati 8:1-40 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Naye Benyamini akamzaa Bela, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Ashbeli, na wa tatu Ahiramu; na wa nne Noha, na wa tano Rafa. Na Bela alikuwa na wana; Adari, na Gera, na Abihudi; na Abishua, na Naamani, na Ahoa; na Gera, na Shufamu, na Huramu. Na hawa ndio wana wa Ehudi. (Hao ndio wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Geba; nao wakawachukua mateka mpaka Manahathi; na Naamani, na Ahoa, na Gera; aliwachukua mateka). Naye akamzaa Uza, na Ahihudi. Na Shaharaimu akazaa watoto katika Bara-Moabu, baada ya kuwafukuza wakeze Hushimu na Baara. Akazaliwa na Hodeshi, mkewe; Yobabu, na Sibia, na Mesha, na Malkamu; na Yeusi, na Shakia, na Mirma. Hao ndio wanawe, wakuu wa mbari za baba zao. Naye alikuwa amezaliwa na Hushimu, Abitubu, na Elpaali. Na wana wa Elpaali; Eberi, na Mishamu, na Shemedi, ambaye ndiye aliyejenga Ono na Lodi, pamoja na vijiji vyake; na Beria, na Shema, waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao miongoni mwa wenyeji wa Aiyaloni, wale ambao waliwakimbiza wenyeji wa Gathi. Na Ahio, na Ghashaki, na Yeremothi; na Zebadia, na Aradi, na Ederi; na Mikaeli, na Ishpa, na Yoha; walikuwa wana wa Beria. Na Zebadia, na Meshulamu, na Hizki, na Heberi; na Ishmerai, na Izlia, na Yobabu; walikuwa wana wa Elpaali. Na Yakimu, na Zikri, na Zabdi; na Elienai, na Silethai, na Elieli; na Adaya, na Beraya, na Shimrathi; walikuwa wana wa Shema. Na Ishpani, na Eberi, na Elieli; na Abdoni, na Zikri, na Hanani; na Hanania, na Elamu, na Anthothiya; na Ifdeya, na Penueli; walikuwa wana wa Shashaki. Na Shamsherai, na Sheharia, na Athalia; na Yaareshia, na Eliya, na Zikri; walikuwa wana wa Yerohamu. Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu. Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, ambaye jina la mkewe aliitwa Maaka; na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni, na Suri, na Kishi, na Baali, na Nadabu; na Gedori, na Ahio, na Zekaria, Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao. Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali. Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika. Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi. Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa; na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli; naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli. Na wana wa Esheki nduguye ni hawa; mzaliwa wake wa kwanza, Ulamu, na wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti. Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini.