Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 7:1-40

1 Mambo ya Nyakati 7:1-40 Biblia Habari Njema (BHN)

Wana wa Isakari walikuwa wanne: Tala, Pua, Yashubu na Shimroni. Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibsamu na Shemueli. Hao walikuwa wakuu wa jamaa za koo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Idadi ya wazawa wao siku za mfalme Daudi ilikuwa 22,600. Uzi alikuwa na mwana mmoja, jina lake Izrahia. Na wana wa Izrahia walikuwa Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia, jumla wanne, na wote walikuwa wakuu wa jamaa. Kwa vile ambavyo wake na watoto wao walikuwa wengi sana, mliweza kupatikana vikosi vya wanajeshi 36,000 kutokana na wazawa wao. Ndugu zao katika jamaa zote za kabila la Isakari walioandikishwa kwa kufuata koo, walikuwa 87,000, na wote walikuwa mashujaa wa vita. Benyamini alikuwa na wana watatu: Bela, Bekeri na Yediaeli. Bela alikuwa na wana watano: Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa zao, na wanajeshi mashujaa. Walioandikishwa kwa kufuata koo, idadi ya wazawa wao ilikuwa 22,034. Bekeri alikuwa na wana tisa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Eliehonai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Wote hawa ni wazawa wa Bekeri. Waliandikishwa kwa koo kulingana na vizazi vyao kama viongozi wa jamaa zao, na idadi ya wazawa wao ilikuwa 20,200, wote wakiwa mashujaa wa vita. Yediaeli alikuwa na mwana mmoja, jina lake Bilhani. Bilhani alikuwa na wana: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. Wote hawa walikuwa wakuu wa jamaa katika koo zao na askari mashujaa wa vita. Kutokana na wazawa wao, kulipatikana wanaume 178,200, wanajeshi hodari tayari kabisa kwa vita. Shupimu na Hupimu pia walikuwa wa kabila hili. Dani alikuwa na mwana mmoja, jina lake Hushimu. Naftali alikuwa na wana wanne: Yaasieli, Guni, Yereri na Shalumu. Hao walikuwa wazawa wa Bilha. Manase alikuwa na wana wawili kutokana na suria wake Mwaramu: Asrieli na Makiri. Makiri alikuwa baba yake Gileadi. Makiri aliwazaa Hupimu na Shupimu. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri alikuwa Selofehadi. Selofehadi alikuwa na mabinti peke yake. Maaka mkewe Makiri, alizaa mwana jina lake Pereshi. Jina la nduguye Pereshi lilikuwa Shereshi. Wanawe Shereshi walikuwa Ulamu na Rakemu. Rakemu alimzaa Bedani. Hawa wote ni wazawa wa Gileadi, mwana wa Makiri, mjukuu wa Manase. Hamo-lekethi, dada yake Gileadi, aliwazaa Ishhodi, Abiezeri na Mala. Wana wa Shemida walikuwa Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu. Hawa ndio wazawa wa Efraimu kutoka kizazi hadi kizazi: Shuthela, Beredi, Tahathi, Eleada, Tahathi, Zabadi na Shuthela. Mbali na Shuthela, Efraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa nchi ya Gathi kwa sababu walikwenda huko kuwanyanganya mifugo yao. Efraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na ndugu zake wakaja kumfariji. Ndipo Efraimu akalala na mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana. Efraimu akampa jina Beria, kwa sababu ya maafa yaliyoipata jamaa yake. Efraimu alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliyeijenga miji ya Beth-horoni ya juu na chini, na Uzen-sheera. Efraimu alimzaa pia Refa ambaye alimzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani, Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama, Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua. Milki zao na makao yao yalikuwa: Betheli na vitongoji vyake, Naraani uliokuwa upande wa mashariki, Gezeri uliokuwa upande wa magharibi pamoja na vitongoji vyake, Shekemu na vitongoji vyake, na Aya na vitongoji vyake. Na pia mipakani mwa wana wa Manase: Beth-sheani na vitongoji vyake, Taanaki na vitongoji vyake, Megido na vitongoji vyake na Dori na vitongoji vyake. Hiyo ndiyo miji walimoishi wazawa wa Yosefu, mwana wa Israeli. Hawa ndio wazawa wa Asheri. Asheri alikuwa na wana wanne: Imna, Ishva, Ishri na Beria, na binti mmoja jina lake Sera. Beria alikuwa na wana wawili: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi. Heberi alikuwa na wana watatu: Yafleti, Shomeri na Hothamu, na binti mmoja jina lake Shua. Yafleti pia alikuwa na wana watatu: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Shemeri, nduguye, alikuwa na wana watatu: Roga, Yehuba na Aramu. Na Helemu, ndugu yake mwingine, alikuwa na wana wanne: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali. Wana wa Sofa walikuwa Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera. Wana wa Yetheri walikuwa Yefune, Pispa na Ara. Wana wa Ula walikuwa Ara, Hanieli na Risia. Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.

1 Mambo ya Nyakati 7:1-40 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne. Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa koo za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita. Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu. Na pamoja nao, katika vizazi vyao, kulingana na koo za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu elfu thelathini na sita; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi. Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu elfu themanini na saba. Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu. Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu elfu ishirini na mbili na thelathini na wanne. Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri. Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu elfu ishirini na mia mbili. Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari. Hao wote ndio wana wa Yediaeli, kulingana na wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, elfu kumi na saba na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi. Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri. Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shalumu; wana wa Bilha. Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi; naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao dada yao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti. Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu. Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase. Na dada yake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala. Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu. Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi; na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuwapokonya ng'ombe wao. Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji. Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu maafa yalikuwa yameipata nyumba yake. Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera. Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani; na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama; na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua. Na hizi ndizo miliki yao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake; na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na dada yao, Sera. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi. Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na dada yao, Shua. Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti. Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu. Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali. Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra; na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera. Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara. Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia. Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa koo za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, viongozi wa wakuu. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu elfu ishirini na sita.

1 Mambo ya Nyakati 7:1-40 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne. Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa mbari za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu ishirini na mbili elfu na mia sita. Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu. Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi. Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu themanini na saba elfu. Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu. Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu ishirini na mbili elfu na thelathini na wanne. Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri. Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu ishirini elfu na mia mbili. Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari. Hao wote ndio wana wa Yediaeli, sawasawa na wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, kumi na saba elfu na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi. Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri. Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shilemu; wana wa Bilha. Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi; naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti. Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu. Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase. Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala. Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu. Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi; na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuzipokonya ng’ombe zao. Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji. Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu mna mabaya nyumbani mwake. Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera. Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani; na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama; na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua. Na hizi ndizo hozi zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake; na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi. Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na umbu lao, Shua. Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti. Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu. Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali. Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra; na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera. Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara. Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia. Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa mbari za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, wakuu wa mashehe. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu ishirini na sita elfu.

1 Mambo ya Nyakati 7:1-40 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Wana wa Isakari walikuwa: Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne. Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600. Mwana wa Uzi alikuwa: Izrahia. Wana wa Izrahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi. Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000. Wana watatu wa Benyamini walikuwa: Bela, Bekeri na Yediaeli. Wana wa Bela walikuwa: Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034. Wana wa Bekeri walikuwa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200. Mwana wa Yediaeli alikuwa: Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani. Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri. Wana wa Naftali walikuwa: Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha. Wana wa Manase walikuwa: Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu. Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu. Mwana wa Ulamu alikuwa: Bedani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase. Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla. Wana wa Shemida walikuwa: Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu. Wana wa Efraimu walikuwa: Shuthela, ambaye alimzaa Beredi, Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada, Eleada akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Zabadi, na Zabadi akamzaa Shuthela. Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera. Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani, Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama, Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua. Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii. Wana wa Asheri walikuwa: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera. Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi. Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao. Wana wa Yafleti walikuwa: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti. Wana wa Shemeri walikuwa: Ahi, Roga, Yehuba na Aramu. Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali. Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera. Wana wa Yetheri walikuwa: Yefune, Pispa na Ara. Wana wa Ula walikuwa: Ara, Hanieli na Risia. Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha