Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 6:31-81

1 Mambo ya Nyakati 6:31-81 Biblia Habari Njema (BHN)

Hawa ndio watu ambao mfalme Daudi aliwaweka wahudumu kama waimbaji katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baada ya sanduku la agano kuwekwa ndani. Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu. Zifuatazo ni koo za wale ambao walitoa huduma hizo: Ukoo wa Kohathi: Hemani, kiongozi wa kundi la kwanza la waimbaji, alikuwa mwana wa Yoeli. Ukoo wake kutokana na Israeli ni kama ifuatavyo: Hemani, mwana wa Yoeli, mwana wa Samueli, mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa, mwana wa Zufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai, mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania, mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli. Asafu, ndugu yake alikuwa upande wake wa kulia. Ukoo wake kutokana na Lawi: Asafu, mwana wa Berekia, mwana wa Shimea, mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya, mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaya, mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei, mwana wa Yahathi, mwana wa Gershomu, mwana wa Lawi. Ethani wa ukoo wa Merari, alikuwa kiongozi wa kundi la tatu la waimbaji. Ukoo wake kutokana na Lawi ni kama ifuatavyo: Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki, mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia, mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri, mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi. Ndugu zao wengine walipewa wajibu wa kuhudumia hema takatifu la nyumba ya Mungu. Aroni na wazawa wake ndio waliokuwa wakitoa tambiko juu ya madhabahu ya tambiko za kuteketezwa na pia juu ya madhabahu ya kufukizia ubani. Walifanya kazi zote zilizohusika na mahali patakatifu sana ili kuifanyia Israeli upatanisho. Haya yote waliyafanya kulingana na maagizo aliyotoa Mose, mtumishi wa Mungu. Wafuatao ndio wazawa wa Aroni: Aroni alimzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Serahia, Serahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi. Yafuatayo ndiyo makazi yao kulingana na mipaka yake: Wazawa wa Aroni katika jamaa ya Wakohathi kulingana na kura yao, hao walipewa mji wa Hebroni katika nchi ya Yuda na malisho kandokando yake. Lakini mashamba ya mjini pamoja na malisho yake alipewa Kalebu mwana wa Yefune. Wazawa wa Aroni walipewa miji ya makimbilio: Hebroni, Libna pamoja na malisho yake, Yatiri na Eshtemoa pamoja na malisho yake, Hileni na Debiri pamoja na malisho yake, Ashani na Beth-shemeshi pamoja na malisho yake. Katika eneo la kabila la Benyamini walipewa miji ya Geba, Alemethi na Anathothi pamoja na malisho ya miji hiyo. Miji yote waliyopewa kulingana na jamaa zao ilikuwa kumi na mitatu. Miji kumi ya eneo la nusu ya kabila la Manase ilitolewa kwa sehemu iliyobaki ya ukoo wa Kohathi kwa kura kulingana na jamaa zao. Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani. Vivyo hivyo, miji kumi na miwili katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi na katika kabila la Zebuluni ilipewa ukoo wa Merari kulingana na jamaa zao. Kwa njia hii watu wa Israeli waliwapa Walawi miji ili waishi humo pamoja na malisho ya miji hiyo. (Miji iliyotajwa majina hapa juu katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni na katika kabila la Benyamini iligawiwa kabila la Lawi kwa kura.) Jamaa nyingine za ukoo wa Kohathi zilipewa miji pamoja na malisho yake katika kabila la Efraimu: Shekemu, mji wa makimbilio katika nchi ya milima ya Efraimu pamoja na malisho yake, Gezeri pamoja na malisho yake, Yokmeamu pamoja na malisho yake, Beth-horoni pamoja na malisho yake; Aiyaloni pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake. Katika nusu ya kabila la Manase walipewa miji ya Aneri pamoja na malisho yake, na Bileamu pamoja na malisho yake. Hii ndiyo miji iliyopewa jamaa za ukoo wa Kohathi. Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: Katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake. Katika kabila la Isakari walipewa: Kedeshi pamoja na malisho yake, Deberathi pamoja na malisho yake, Ramothi pamoja na malisho yake na Anemu pamoja na malisho yake. Katika kabila la Asheri walipewa: Mashali pamoja na malisho yake, Abdoni pamoja na malisho yake, Hukoki pamoja na malisho yake, na Rehobu na malisho yake. Katika kabila la Naftali: Kedeshi katika Galilaya pamoja na malisho yake, Hamoni pamoja na malisho yake na Kiriathaimu pamoja na malisho yake. Jamaa za Merari zilizosalia, zilipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake kandokando ya miji hiyo: Katika kabila la Zebuluni walipewa Rimono pamoja na malisho yake na Tabori pamoja na malisho yake. Katika kabila la Reubeni, mashariki ya mto Yordani karibu na mji wa Yeriko walipewa Bezeri ulioko katika nyanda za juu pamoja na malisho yake, Yahasa pamoja na malisho yake, Kedemothi pamoja na malisho yake na Mefaathi pamoja na malisho yake. Katika kabila la Gadi walipewa Ramothi katika Gileadi pamoja na malisho yake, Mahanaimu pamoja na malisho yake, Heshboni pamoja na malisho yake na Yazeri pamoja na malisho yake.

1 Mambo ya Nyakati 6:31-81 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi kwenye kazi ya kuimba katika nyumba ya BWANA, sanduku lile lilipopata mahali pa kukaa. Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; nao wakatoa huduma yao kwa kufuata zamu zao. Na hawa ndio waliohudumu pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli; mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu; mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai; mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli; mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli. Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kulia, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea; mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya; mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido; mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei; mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi. Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki; mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia; mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri; mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi. Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu. Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, kulingana na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu. Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua; na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia; na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu; na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi. Basi haya ndiyo makao yao, kwa kufuata mipaka ya kambi zao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza; wakapewa Hebroni, katika nchi ya Yuda, na vijiji vyake vilivyouzunguka; bali mashamba ya mji huo, na vijiji vyake, alipewa Kalebu, mwana wa Yefune. Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake; na Holoni pamoja na viunga vyake, na Debiri pamoja na viunga vyake; na Ashani pamoja na viunga vyake, na Beth-shemeshi pamoja na viunga vyake; tena katika kabila la Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu. Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hilo, yaani, nusu kabila, nusu ya Manase. Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, kulingana na jamaa zao, katika kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika kabila la Manase waliokaa Bashani. Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, kulingana na jamaa zao, katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi, na katika kabila la Zabuloni. Na wana wa Israeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na viunga vyake. Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila la wana wa Yuda, na katika kabila la wana wa Simeoni, na katika kabila la wana wa Benyamini. Na jamaa nyingine za wana wa Kohathi walikuwa na miji ya mipakani mwao katika kabila la Efraimu. Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake; na Yokmeamu pamoja na viunga vyake, na Beth-horoni pamoja na viunga vyake; na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake; na katika nusu kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi. Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake; na katika kabila la Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake; na Remethi pamoja na viunga vyake, na En-gaminu pamoja na viunga vyake; na katika kabila la Asheri; Mishali pamoja na viunga vyake, na Abdoni pamoja na viunga vyake; na Helkathi pamoja na viunga vyake, na Rehobu pamoja na viunga vyake; na katika kabila la Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake. Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila la Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake; na ng'ambo ya mto wa Yordani huko Yeriko, upande wa mashariki wa Yordani, katika kabila la Reubeni; Bezeri katika nyika pamoja na viunga vyake, na Yahasa pamoja na viunga vyake, na Kedemothi pamoja na viunga vyake, na Mefaathi pamoja na viunga vyake; na katika kabila la Gadi; Ramothi katika Gileadi pamoja na viunga vyake, na Mahanaimu pamoja na viunga vyake; na Heshboni pamoja na viunga vyake, na Yazeri pamoja na viunga vyake.

1 Mambo ya Nyakati 6:31-81 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi juu ya kazi ya kuimba katika nyumba ya BWANA, sanduku lile lilipokwisha pata mahali pa kustarehe. Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao. Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli; mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu; mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai; mwana wa Elkana, mwana wa Shauli, mwana wa Uzia, mwana wa Urieli; mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora; mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli. Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kuume, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea; mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya; mwana wa Yeatherai, mwana wa Zera, mwana wa Ido; mwana wa Yoa, mwana wa Zima, mwana wa Shimei; mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi. Na upande wa kushoto ndugu zao, wana wa Merari; Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki; mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia; mwana wa Amzi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri; mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi. Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu. Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu. Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua; na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia; na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu; na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi. Basi haya ndiyo makao yao, sawasawa na marago yao mipakani mwao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza; wakapewa Hebroni, katika nchi ya Yuda, na vijiji vyake vilivyouzunguka; bali mashamba ya mji huo, na vijiji vyake, alipewa Kalebu, mwana wa Yefune. Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake; na Holoni pamoja na viunga vyake, na Debiri pamoja na viunga vyake; na Ashani pamoja na viunga vyake, na Beth-shemeshi pamoja na viunga vyake; tena katika kabila ya Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu. Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hiyo, yaani, nusu-kabila, nusu ya Manase. Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani. Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Reubeni, na katika kabila ya Gadi, na katika kabila ya Zabuloni. Na wana wa Israeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na viunga vyake. Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila ya wana wa Yuda, na katika kabila ya wana wa Simeoni, na katika kabila ya wana wa Benyamini. Na jamaa nyingine za wana wa Kohathi walikuwa na miji ya mipakani mwao katika kabila ya Efraimu. Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake; na Yokmeamu pamoja na viunga vyake, na Beth-horoni pamoja na viunga vyake; na Aiyaloni pamoja na viunga vyake, na Gath-rimoni pamoja na viunga vyake; na katika nusu-kabila ya Manase; Taanaki pamoja na viunga vyake, na Ibleamu pamoja na viunga vyake; kwa mabaki ya jamaa ya wana wa Kohathi. Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu-kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake; na katika kabila ya Isakari; Kishioni pamoja na viunga vyake, na Daberathi pamoja na viunga vyake; na Remethi pamoja na viunga vyake, na En-gaminu pamoja na viunga vyake; na katika kabila ya Asheri; Mishali pamoja na viunga vyake, na Abdoni pamoja na viunga vyake; na Helkathi pamoja na viunga vyake, na Rehobu pamoja na viunga vyake; na katika kabila ya Naftali; Kedeshi katika Galilaya pamoja na viunga vyake, na Hamothi pamoja na viunga vyake, na Kiriathaimu pamoja na viunga vyake. Nao mabaki ya Walawi, wana wa Merari, wakapewa, katika kabila ya Zabuloni; Rimona pamoja na viunga vyake, na Tabori pamoja na viunga vyake; na ng’ambo ya mto wa Yordani huko Yeriko, upande wa mashariki wa Yordani, katika kabila ya Reubeni; Bezeri katika nyika pamoja na viunga vyake, na Yahasa pamoja na viunga vyake, na Kedemothi pamoja na viunga vyake, na Mefaathi pamoja na viunga vyake; na katika kabila ya Gadi; Ramothi katika Gileadi pamoja na viunga vyake, na Mahanaimu pamoja na viunga vyake; na Heshboni pamoja na viunga vyake, na Yazeri pamoja na viunga vyake.

1 Mambo ya Nyakati 6:31-81 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba ya BWANA, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko. Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu la BWANA huko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa. Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao: Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa: Hemani, mpiga kinanda, alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli, mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa, mwana wa Sufu, mwana wa Elikana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai, mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania, mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli; na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume: Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea, mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya, mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaya, mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei, mwana wa Yahathi, mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi. Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto: Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki, mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia, mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri, mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi. Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu. Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni: Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia, Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi. Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka. Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune. Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa, Hileni, Debiri, Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho. Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi. Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase. Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani. Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni. Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho. Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu. Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu. Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri, Yokmeamu, Beth-Horoni, Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho. Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho. Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: Katika nusu ya kabila la Manase: walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi. Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi, Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho. Kutoka kabila la Asheri walipokea Mashali, Abdoni, Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho. Kutoka kabila la Naftali walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho. Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo: kutoka kabila la Zabuloni walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho. Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa, Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho. Na kutoka kabila la Gadi walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu, Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.