1 Mambo ya Nyakati 22:11-13
1 Mambo ya Nyakati 22:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Sasa mwanangu, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako na awe pamoja nawe ili ufaulu kumjengea nyumba kama alivyosema. Mwenyezi-Mungu akupe busara na akili ili atakapokupa uongozi juu ya Israeli, uzishike sheria zake Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Ukiwa mwangalifu, na ukizitii amri ambazo Mwenyezi-Mungu alimwagiza Mose juu ya Israeli, utastawi. Jipe moyo, uwe imara. Usiogope wala usifadhaike.
1 Mambo ya Nyakati 22:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sasa mwanangu, BWANA na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya BWANA, Mungu wako, kama alivyonena kuhusu habari zako. BWANA na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike Torati ya BWANA, Mungu wako. Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, BWANA alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.
1 Mambo ya Nyakati 22:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sasa mwanangu, BWANA na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya BWANA, Mungu wako, kama alivyonena kwa habari zako. BWANA na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike torati ya BWANA, Mungu wako. Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, BWANA alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.
1 Mambo ya Nyakati 22:11-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Sasa, mwanangu, BWANA awe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba ya BWANA Mungu wako, kama alivyosema utafanya. BWANA na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria ya BWANA Mungu wako. Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheria BWANA alizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.