Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 36:5-10

Zaburi 36:5-10 BHN

Fadhili zako ee Mwenyezi-Mungu zaenea hata mbinguni; uaminifu wako wafika mawinguni. Uadilifu wako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama vilindi vya bahari. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama Jinsi gani zilivyo bora fadhili zako! Wanadamu hukimbilia kivulini mwa mabawa yako. Wawashibisha kwa utajiri wa nyumba yako; wawanywesha kutoka mto wa wema wako. Wewe ndiwe asili ya uhai; kwa mwanga wako twaona mwanga. Uendelee kuwafadhili wale wanaokutambua; uzidi kuwa mwema kwa wanyofu wa moyo.

Soma Zaburi 36