Mwanangu, ule asali maana ni nzuri; sega la asali ni tamu mdomoni. Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako; ukiipata utakuwa na matazamio mema, wala tumaini lako halitakuwa la bure. Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema, wala usijaribu kuiharibu nyumba yake, maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga. Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake, maana Mwenyezi-Mungu aonaye hayo hatapendezwa; huenda akaacha kumwadhibu. Usihangaike kwa sababu ya watenda mabaya, wala usiwaonee wivu watu waovu, maana mwovu hatakuwa na mema baadaye; taa ya uhai wake itazimwa. Mwanangu, umche Mwenyezi-Mungu na kumheshimu mfalme, wala usishirikiane na wale wasio na msimamo, maana maangamizi yao huwapata ghafla. Hakuna ajuaye maafa watakayozusha.
Soma Methali 24
Shirikisha
Linganisha Matoleo Yote: Methali 24:13-22
Hifadhi mistari, soma bila mtandao, tazama klipu za mafunzo, na zaidi!
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video