Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 23:19-25

Methali 23:19-25 BHN

Sikia mwanangu, uwe na hekima; fikiria sana jinsi unavyoishi. Usiwe mmoja wa walevi wa divai, wala walafi wenye kupenda nyama, maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini, anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara. Msikilize baba yako aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako akizeeka. Nunua ukweli, wala usiuuze; nunua hekima, mafunzo na busara. Baba wa mtoto mwadilifu atajaa furaha; anayemzaa mtoto mwenye hekima atamfurahia. Wafurahishe baba na mama yako; mama aliyekuzaa na afurahi.

Soma Methali 23

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Methali 23:19-25