Hesabu 27:18-20
Hesabu 27:18-20 BHN
Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mtwae Yoshua mwana wa Nuni, mtu mwenye roho nzuri, kisha umwekee mikono, na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na jumuiya yote, umkabidhi jukumu hilo. Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli imtii.