Mathayo 19:16-21
Mathayo 19:16-21 BHN
Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye kitu gani chema ili niupate uhai wa milele?” Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uhai, shika amri.” Yule mtu akamwuliza, “Amri zipi?” Yesu akasema, “Usiue, Usizini, Usiibe, Usitoe ushahidi wa uongo, Waheshimu baba yako na mama yako; na, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” Huyo kijana akamwambia, “Hayo yote nimeyazingatia; nifanye nini zaidi?” Yesu akamwambia, “Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako, uwape maskini fedha hiyo, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.”