Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 14:25-35

Luka 14:25-35 BHN

Hapo, makundi mengi yakawa yanaandamana pamoja na Yesu. Basi, akawageukia watu akawaambia, “Mtu yeyote akija kwangu, asipomchukia baba yake, mama yake, mke wake, watoto, ndugu na dada zake, naam, hata na nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu asiyechukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi cha kutosha cha kumalizia? La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka wakisema: ‘Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.’ “Au, ni mfalme gani ambaye akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza na kufikiri kama ataweza, kwa askari wake10,000, kumkabili yule aliye na askari 20,000? Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali. Vivyo hivyo, basi, hakuna hata mmoja wenu atakayekuwa mwanafunzi wangu kama asipoachilia kila kitu alicho nacho. “Chumvi ni nzuri; lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? Haifai kitu wala kwa udongo wala kwa mbolea. Watu huitupilia mbali. Mwenye masikio na asikie!”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 14:25-35

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha