Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohane 11:17-26

Yohane 11:17-26 BHN

Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne. Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu, umbali upatao kilomita tatu. Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao. Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani. Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa! Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.” Yesu akamwambia, “Kaka yako atafufuka.” Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi; na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yohane 11:17-26