Isaya 10:1-3
Isaya 10:1-3 BHN
Ole wao wanaotunga sheria zisizo za haki, watu wanaopitisha sheria za kukandamiza. Huwanyima maskini haki zao, na kuwaibia maskini wa watu wangu maslahi yao. Wajane wamekuwa nyara kwao; yatima wamekuwa mawindo yao. Je, mtafanya nini siku ya adhabu, siku dhoruba itakapowajieni kutoka mbali? Mtamkimbilia nani kuomba msaada? Mtakwenda wapi kuweka mali yenu?