Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wathesalonike 1:1-4

1 Wathesalonike 1:1-4 BHN

Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani. Tunamshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi nyote na kuwakumbukeni daima katika sala zetu. Maana, mbele ya Mungu Baba yetu, twakumbuka jinsi mnavyoonesha imani yenu kwa matendo, jinsi upendo wenu unavyowawezesha kufanya kazi kwa bidii, na jinsi tumaini lenu katika Bwana wetu Yesu Kristo lilivyo thabiti. Ndugu, twajua kwamba Mungu anawapenda na kwamba amewateua muwe watu wake

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 Wathesalonike 1:1-4