1 Wakorintho 10:15-17
1 Wakorintho 10:15-17 BHN
Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo. Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.