Mwanzo 24:3-4
Mwanzo 24:3-4 ONMM
Ninataka uape kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke kutoka binti za Wakanaani, ambao ninaishi miongoni mwao. Bali nenda katika nchi yangu na jamaa zangu umpatie Isaka mwanangu mke.”