Yohana 20
20
Maria Magadalene kaburini.
(1-18: Mat. 28:1-10; Mar. 16:1-11; Luk. 24:1-12.)
1Siku ya kwanza ya juma Maria Magadalene akaenda mapema kaburini, kukingali gizagiza. Alipoliona lile jiwe, limekwisha ondolewa kaburini, 2akapiga mbio, akamwendea Simoni Petero na yule mwanafunzi mwingine, Yesu aliyempenda, akawaambia: Wamemwondoa Bwana kaburini, nasi hatujui, walikomweka.#Yoh. 13:23. 3Ndipo, Petero na yule mwanafunzi mwingine walipoondoka kwenda kaburini, 4wote wawili wakipiga mbio pamoja; lakini yule mwanafunzi mwingine akaja mbele kwa mbio, akamshinda Petero, akafika wa kwanza penye kaburi. 5Akainama, akachungulia, akaiona sanda, imewekwa, lakini hakuingia. 6Kisha Simoni Petero akafika akimfuata, akaingia kaburini, akaiona sanda, imewekwa; 7lakini mharuma uliokuwa kichwani pake haukuwekwa pamoja na sanda, ila ulikuwa umekunjwa na kuwekwa mahali pake peke yake.#Yoh. 11:44. 8Ndipo, alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyefika wa kwanza penye kaburi, akaviona, akavisadiki. 9Kwani hawajayajua bado yaliyoandikwa kwamba: Imempasa kufufuka katika wafu.#Tume. 2:24-32; 1 Kor. 15:4. 10Kisha wale wanafunzi wakarudi tena kwao.
11*Lakini Maria alikuwa amesimama nje penye kaburi akilia. Basi, alipokuwa akilia, akainama kuchungulia kaburini, 12akaona malaika wawili wenye nguo nyeupe, wamekaa hapo, mwili wa Yesu ulipokuwa umewekwa, mmoja kichwani, mmoja miguuni. 13Hao walipomwuliza: Mama, waliliani? akawaambia: Maana wamemwondoa Bwana wangu, nami sijui, walikomweka. 14Alipoyasema hayo akageuka nyuma, akamwona Yesu, amesimama, lakini hakujua, ya kuwa ndiye Yesu. 15Yesu alipomwambia: Mama, waliliani? Wamtafuta nani? alidhani, ni mlinzi wa kiunga, akamwambia: Bwana, kama wewe umemchukua, niambie, ulikomweka, nipate kwenda, nimchukue! 16Yesu akamwambia: Maria! Ndipo, alipogeuka, akamwambia Kiebureo: Rabuni! maana yake: Mfunzi mkuu! 17Yesu akamwambia: Usiniguse! Kwani sijapaa bado kwenda kwake Baba. Lakini uende kwa ndugu zangu, uwaambie: Ninapaa kwenda kwa Baba yangu aliye hata Baba yenu na kwa Mungu wangu aliye hata Mungu wenu.#Ebr. 2:11-12. 18Maria Magadalene akaenda, akawasimulia wanafunzi: Nimemwona Bwana, tena hayo ndiyo, aliyoniambia.*
Wanafunzi pasipo Toma.
(19-23: Mar. 16:14-18; Luk. 24:36-49.)
19*Siku ile ya kwanza ya juma kulipokuchwa, wanafunzi wakakutana, milango ya mle walimokuwa ikiwa imefungwa, maana waliwaogopa Wayuda. Mara Yesu akaja, akasimama katikati, akawaambia: Tengemaneni!#Luk. 24:36. 20Naye alipokwisha kuyasema haya akawaonyesha maganja na ubavu. Wanafunzi walipomwona Bwana wakafurahi.#1 Yoh. 1:1. 21Yesu akawaambia tena: Tengemaneni! Kama Baba alivyonituma mimi, ndivyo, nami ninavyowatuma ninyi.#Yoh. 17:18. 22Naye alipokwisha kuyasema haya, akawapuzia, akawaambia: Pokeeni Roho takatifu! 23Watu, mtakaowaondolea makosa, watakuwa wameondolewa. Nao watu, mtakaowafungia, watakuwa wamefungiwa.#Mat. 16:19; 18:18.
Wanafunzi pamoja na Toma.
24Lakini Toma anayeitwa Pacha aliyekuwa mmoja wao wale kumi na wawili hakuwamo pamoja nao, Yesu alipokuja.#Yoh. 11:16; 14:5. 25Wanafunzi wenzake walipomwambia: Tumemwona Bwana! akawajibu: Nisipoyaona makovu ya misumari maganjani mwake na kukitia kidole changu pale penye misumari, tena nisipoutia mkono wangu ubavuni mwake, sitamtegemea.#Yoh. 19:34. 26Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo tena, naye Toma alikuwa yumo pamoja nao. Yesu akaja, milango ilipokuwa imefungwa, akasimama katikati, akasema: Tengemaneni!#Yoh. 20:19. 27Kisha akamwambia Toma: Lete kidole chako hapa, uyatazame maganja yangu! Lete nao mkono wako, uutie ubavuni mwangu! Usiwe mtu asiyenitegemea, ila anitegemeaye! 28Ndipo, Toma alipomjibu, akamwambia: Bwana wangu na Mungu wangu!#Yoh. 1:1. 29Yesu akamwambia: Umenitegemea, kwa sababu umeniona. Wenye shangwe ndio wanitegemeao pasipo kuona!#1 Petr. 1:8.
30Viko vielekezo vingi vingine, Yesu alivyovifanya mbele ya wanafunzi, visivyoandikwa katika kitabu hiki.#Yoh. 21:24-25. 31Lakini hivyo vimeandikwa, mpate kuyategemea, ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wake Mungu, tena mpate uzima katika Jina lake kwa kumtegemea.*#1 Yoh. 5:13.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 20: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.