Yohana 16:7-8
Yohana 16:7-8 SRB37
Lakini mimi nawaambiani lililo la kweli: Inawafalia, mimi niende zangu. Kwani nisipokwenda zangu, mtuliza mioyo hatawajia. Lakini nitakapokwenda, nitamtuma kwenu. Naye atakapokuja atawaumbua wao wa ulimwengu kuwa wenye makosa wasio nalo la kujikania, wanaopaswa na kuhukumiwa.