Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 3

3
Kiwete.
1*Petero na Yohana wakapanda kwenda Patakatifu saa tisa, watu walipoombea. 2Kulikuwa na mtu aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mama yake; naye huchukuliwa, awekwe kila siku karibu ya mlango wa Patakatifu unaoitwa Mzuri, aombe sadaka kwao wanaoingia Patakatifu.#Tume. 14:8. 3Alipomwona Petero na Yohana, wakitaka kupaingia Patakatifu, akataka kupewa sadaka nao. 4Lakini Petero akamkazia macho pamoja na Yohana, akasema: Tutazame sisi! 5Alipowatumbulia macho akingoja, watakachompa, 6Petero akasema: Fedha na dhahabu sinazo, lakini nilicho nacho, nitakupa. Katika Jina la Yesu Kristo wa Nasareti inuka, uende!#Tume. 3:16. 7Kisha akamshika mkono wa kuume, akamwinua. Papo hapo miguu yake na fundo zake zikapata nguvu, 8akaruka, akasimama, akaenda, akapaingia Patakatifu pamoja nao akizunguka na kurukaruka na kumsifu Mungu. 9Watu wote walipomwona, anavyozunguka na kumsifu Mungu, 10wakamtambua, ya kuwa huyu ndiye aliyekaa na kuomba sadaka karibu ya Mlango Mzuri wa Patakatifu. Wote wakashangaa mno na kuyastukia yale yaliyompata.
Matangazo ya Petero.
11Aliposhikamana na Petero na Yohana, watu wote wakawakusanyikia mbio katika ukumbi unaoitwa wa Salomo kwa kushangaa.#Tume. 5:12; Yoh. 10:23. 12Petero alipowaona akawaambia wale watu: Waume Waisiraeli, haya mnayashangaaje? Nasi mnatutumbualiaje macho, kama ni nguvu yetu sisi, au kama ni hivyo, tunavyomcha Mungu, vinavyomwendesha huyu? 13Mungu wa Aburahamu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu wa kele, amemtukuza mtoto wake Yesu, ninyi mliyemtoa na kumkana mbele ya Pilato, alipokata shauri, kwamba afunguliwe.#Tume. 2:23; 5:30; Yes. 53:11. 14Lakini ninyi mkamkana aliyekuwa mtakatifu na mwongofu, mkataka kupewa aliyekuwa mwuaji,#Mat. 27:20-21. 15mwenye kuwaongoza uzimani mkamwua. Lakini Mungu amemfufua katika wafu, nasi ndio mashahidi.#Tume. 4:10. 16Tena kwa hivyo, huyu alivyolitegemea Jina lake, hilo Jina lake limemtia nguvu huyu, mnayemwona na kumjua. Kweli hivyo, alivyolitegemea kwa kutiwa nguvu nalo, ndivyo vilivyompa huu uzima wote, mnaouona ninyi nyote.* 17Sasa, ndugu zangu, ninajua, ya kuwa mliyafanya pasipo kujua maana, kama wakubwa wenu nao.#Luk. 23:34. 18Lakini hivyo ndivyo, Mungu alivyoyatimiza, aliyoyatangaza kale kwa vinywa vya wafumbuaji wote kwamba: Kristo wake atateswa.#Luk. 24:27. 19Kwa hiyo juteni na kugeuka, makosa yenu yafutwe, yawatoke!#Tume. 2:38. 20Ndipo, zitakapowafikia nazo siku za kupoea usoni pa Bwana, tena ndipo, atakapopata kumtuma Kristo Yesu, mliyepewa kwanza. 21Ndiye, aliyempasa kuutwaa ufalme wa mbingu, mpaka siku zifike, vitu vyote vitakaporudishiwa upya, kama Mungu alivyosema hata kale kwa vinywa vya wafumbuaji wake watakatifu. 22Mose alisema:
Miongoni mwa ndugu zenu Bwana Mungu atawainulia mfumbuaji
atakayelingana na mimi, nanyi sharti mmsikie yote,
atakayowaambia!#5 Mose 18:15,19.
23Lakini itakuwa, kila mtu atakayekataa kumsikia yule
mfumbuaji ataangamizwa, atengwe kabisa nao watu wa kwetu.
24Nao wafumbuaji wote toka kwa Samueli na wale waliofuata, wo wote waliosema, wamepiga mbiu za siku hizo. 25Ninyi m wana wao wafumbuaji, tena m wana wa Agano, Mungu aliloliagana na baba zenu alipomwambia Aburahamu:
Katika uzao wako ndimo,
mataifa yote ya nchi yatakamobarikiwa.#1 Mose 22:18. 26Ninyi m wa kwanza, Mungu aliowafufulia mtoto wake na kumtuma, awabariki, mgeuke kila mmoja mkiyaepuka mabaya yenu.#Tume. 13:46.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 3: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia