Matendo ya Mitume 1
1
Kupaa mbinguni.
1*Mwenzangu Teofilo, katika kitabu cha kwanza nalikuandikia yote, Yesu aliyoanza kuyafanya na kuyafundisha#Luk. 1:3. 2mpaka siku ile, alipopazwa mbinguni. Hapo alikuwa amekwisha kuwaagizia mitume, aliowachagua, mambo ya Roho takatifu.#Luk. 6:13. 3Tena wale ndio, aliowatokea na kuwaonyesha mara kwa mara, ya kuwa anaishi, alipokuwa amekwisha kuteswa; zile siku za kuwaonekea na kusema nao mambo ya ufalme wa Mungu zilikuwa 40. 4Alipokwisha kuwakusanya akawaagiza, wasitoke Yerusalemu, ila wakingoje kiagio cha Baba, mlichokisikia kwangu;#Luk. 24:49; Yoh. 15:26. 5kwani Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho takatifu, tena siku hizo zinazosalia ni chache tu.#Mat. 3:11.
6Waliokusanyika walipomwuliza: Bwana, siku hizo ndipo, utakapowasimamishia Waisiraeli ufalme wao tena?#Luk. 24:21. 7akawaambia: Si nyie waliopaswa na kutambua siku au saa, Baba alizoziweka kwa nguvu yake yeye;#Mat. 24:36; Mar. 13:32. 8ila mtapewa nguvu, Roho Mtakatifu atakapowashukia ninyi, kisha mtakuwa mashahidi wangu hapa Yerusalemu na katika nchi yote ya Yudea na ya Samaria, mfike hata mapeoni kwa nchi. 9Naye alipokwisha kuyasema haya akainuliwa juu, wakitazama, wingu lilivyomchukua machoni pao.#Mar. 16:19; Luk. 24:51; Yoh. 6:62. 10Walipokuwa wakitumbuliza macho mbinguni, alikokwenda, mara waume wawili wenye nguo nyeupe wakasimama huko kwao,#Luk. 24:4. 11nao wakasema: Nyie waume wa Galilea, mmesimamaje mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kwenu na kupazwa mbinguni atarudi vivyo hivyo, mlivyomwona, akienda zake mbinguni.*#Luk. 21:27.
Majina ya mitume.
12Ndipo, walipoondoka penye huo mlima unaoitwa Wa Michekele, ulioko karibu ya Yerusalemu, ni mwendo usio na mwiko wa siku ya mapumziko; wakarudi Yerusalemu.#Luk. 24:50,52-53. 13Walipokwisha ingia wakapanda kipaani mle walimokaa, ni Petero na Yohana na Yakobo na Anderea, Filipo na Toma, Bartolomeo na Mateo, Yakobo wa Alfeo na Simon Zelote na Yuda wa Yakobo.#Luk. 6:13-16. 14Hao wote walishikamana na kutenda moyo mmoja wa kumwomba Mungu, wakawa pamoja na wale wanawake na Maria, mamake Yesu, na pamoja na ndugu zake.#Tume. 2:1; Yoh. 7:3,5.
Matia.
15Siku zile Petero aliinuka katikati ya ndugu waliokuwa wamekutana pamoja, wapata 120, akasema: 16Waume ndugu zangu, ilipasa andiko litimie, Roho Mtakatifu alilolisema kale kinywani mwa Dawidi kwa ajili ya Yuda aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yasu.#Sh. 41:10. 17Kwani alikuwa amehesabiwa pamoja nasi, tena huu utumishi wetu ulikuwa bia moja naye. 18Huyo amepata konde kwa mshahara wa upotovu, akaanguka kifudifudi, akatumbuka katikati, nayo matumbo yake yote yakatoka.#Mat. 27:3-10. 19Vikatambulikana kwa wenyeji wote wa Yerusalemu, wakaliita konde lile kwa msemo wao Hakeldama, ni kwamba: Konde la Damu. 20Kwani imeandikwa katika kitabu cha Mashangilio:
Kao lake liwe hame tu, asioneke atakayetua mlemle.
Tena:
Mtu mwingine na autwae ukaguzi wake.#Sh. 69:26; 109:8. 21Basi, wako wenzetu waliokuwa pamoja nasi siku zote, Bwana Yesu alipoingia kwetu,#Yoh. 15:27. 22mpaka alipotoka tena, tangu hapo, Yohana alipobatiza, mpaka siku ile, alipopazwa na kutolewa kwetu; inapasa, mmoja wao awe shahidi wa ufufuko wake pamoja nasi. 23Wakasimamisha wawili: Yosefu aliyeitwa Barsaba, aliyekuwa na jina jingine la Yusto, na Matia. 24Kisha wakamwomba Mungu wakisema: Wewe Bwana, uitambuaye mioyo yao wote, tuonyeshe mmoja, uliyemchagua katika hawa wawili, 25aupokee huu utumishi na utume, apashike mahali, Yuda alipotoka, aende zake mahali pake yeye. 26Walipowapigia kura, kura ikamguia Matia; kwa hiyo akahesabiwa pamoja na wale mitume kumi na mmoja.#Fano. 16:33.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo ya Mitume 1: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.