Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Sefania 3

3
Uovu wa Yerusalemu
1Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu! 2#Yer 22:21; 5:3 Hakuitii sauti; hakukubali kurudiwa; hakumwamini BWANA; hakumkaribia Mungu wake. 3Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi. 4#Yer 23:11; Eze 22:26 Manabii wake ni watu hafifu, wadanganyifu; makuhani wake wamepatia unajisi patakatifu, wameifanyia sheria udhalimu. 5#Kum 32:4; Zab 99:3,4 BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya. 6Nimekatilia mbali mataifa, minara yao ina ukiwa; nimeziharibu njia kuu zao, hata hapana mmoja apitaye; miji yao imeangamizwa; hamna mtu hata mmoja, wala hapana akaaye huko. 7#Mwa 6:12 Nilisema, Hakika utaniogopa, utakubali kurudiwa; ili yasikatiliwe mbali makao yake, sawasawa ya yote niliyoagiza katika habari zake; lakini waliondoka mapema na kuyaharibu matendo yao yote.
Adhabu na wokovu wa mataifa
8 # Mit 20:22; Yoe 3:2 Basi ningojeeni, asema BWANA, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu.
9Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliitia jina la BWANA, wamtumikie kwa nia moja. 10#Zab 68:31; Mal 1:11; Mdo 8:27 Maana toka nchi iliyo mbali na mito ya Kushi, waniombao dua, yaani, binti za watu wangu waliotawanyika, wataleta matoleo yangu. 11#Mt 3:9 Siku ile hutaaibishwa kwa matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaojigamba na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu. 12#Isa 14:32; 57:15; Mt 5:3; Lk 6:20 Lakini nitabakiza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA. 13#Ufu 14:5 Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautakuwa kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewatisha.
Wimbo wa shangwe
14 # Zab 14:7 Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli;
Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.
15 # Yn 1:49; Eze 48:35; Ufu 21:3 BWANA ameziondoa hukumu zako,
Amemtupa nje adui yako;
Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yuko katikati yako;
Hutaogopa uovu tena.
16 # Isa 35:3 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,
Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.
17BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa;
Atakushangilia kwa furaha kuu,
Atakutuliza katika upendo wake,
Atakufurahia kwa kuimba.
18 # Omb 2:6 Nitawakusanya wanaousikitikia mkutano wa ibada, hao waliokuwa wa kwako; ambao mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa fedheha kwao. 19Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya msifiwe na kujulikana, hao ambao aibu yao ilikuwa katika dunia yote. 20#Zab 22:27 Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi msifiwe na mjulikane, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Sefania 3: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia