Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 2:1-7

Ufunuo 2:1-7 SRUV

Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kulia, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Ninayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wanaojiita mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakini una jambo hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo mimi pia nayachukia. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.

Soma Ufunuo 2

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ufunuo 2:1-7