Ufunuo 12:3-4
Ufunuo 12:3-4 SRUV
Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, lilikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake unakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, limle mtoto wake.