Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 24:1-10

Zaburi 24:1-10 SRUV

Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiweka nafsi yake katika uongo, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari, BWANA hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Soma Zaburi 24

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 24:1-10