Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 103:7-14

Zaburi 103:7-14 SRUV

Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake. BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatashutumu daima, Wala hatashika hasira yake milele. Hakututenda kulingana na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

Soma Zaburi 103

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 103:7-14